Amos 4:7-8


7 a“Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu
kabla ya kufikia mavuno.
Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja,
lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine.
Shamba moja lilipata mvua,
na lingine halikupata, nalo likakauka.

8 bWatu walitangatanga mji hata mji kutafuta maji,
lakini hawakupata ya kuwatosha kunywa,
hata hivyo hamjanirudia mimi,”
asema Bwana.

Copyright information for SwhKC